Azam FC yapepea kwa ushindi wa 1-0 dhidi Mtibwa Sugar

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC  imefanikiwa kuchomoza na ushindi mwembamba wa bao 1 – 0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Azam FC imefanikiwa kupata bao lake la mapema kupitia kwa mchezaji wake, Shaban Idd dakika ya 38 akipokea pasi safi kutoka kwa Ramadhan Singano na hivyo kuwafanya matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam kuzidi kujiimarisha nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad