Bodi ya Ligi Kuchunguza Mechi ya Yanga na Mbeya City

Ikiwa imepita siku moja tokea kulipomalizika kuchezwa kwa mechi kati ya Mbeya City na Yanga hapo jana, Bodi ya ligi nchini (TPLB) imesema inasubiri kupokea ripoti ya mchezo huo ili waweze kupitia kwa makini matukio mbalimbali yaliyojitokeza ikiwemo suala la malalamiko waliyoyatoa kwa Yanga
Hayo yameelezwa na Mtendaji mkuu wa Bodi hiyo Boniface Wambura na kusema suala la Yanga wameshalisikia lakini wanachosubiri wao ni ripoti ambayo itaweza kutoa mwangaza wa kuona tukio zima la wachezaji kuwa wengi uwanjani wa Mbeya City kama walivyodai walalamikaji ambao ni Yanga na mwishowe waweze kukaa kikao kwa mujibu wa kanuni ili kuweza kufanya maamuzi.
"Mechi imechezwa na Ligi yetu bahati nzuri inaonekana. Waamuzi wataleta ripoti pamoja na kamishna wa mchezo na hata msimamizi wa kituo kwa hiyo baada ya kupokea ripoti kuna vikao tutakaa kupitia ripoti na kufanya maamuzi pale tutakapokuta kuna changamoto au matatizo. Lakini vile vile taratibu zipo za kwa watu wenye malalamiko au wenye kutaka kukata rufaa zipo taratibu za kikanuni na tunawaomba wale wote wenye malalamiko wayatume kwa kufuata kanuni", amesema Wambura.#
Kwa upande mwingine, Wambura amesema kwa kuwa yeye ni sehemu ya wenye kikao hicho hawezi kusema sheria inasema nini mpaka pale watakapopitia ili kuhakikisha wanaangalia kanuni zinaelekeza nini kwa suala linalodaiwa kutokea katika mchezo huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad