Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Rukwa, Aida Joseph Kenan amehoji bungeni mjini Dodoma kuhusu ununuzi wa ndege mpya ya Bombadier Q400 aliyoipokea Mhe. Rais Magufuli hivi karibuni, iwapo ndicho kipaumbele cha taifa la Tanzania
Mhe. Aida amesema kwamba ingekuwa vyema kama serikali ingenunua meli na kuzitawanya sehemu mbalimbali nchini kwani wananchi wengi wa hali ya chini waliopo vijijini wanatumia meli katika kusafirisha mazao na shughuli zao zingine na hawana uwezo wa kupanda ndege.
Aidha, amewataka mawaziri kumshauri Rais na Bunge kuisimamia serikali kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote.
Nchi inahitaji pesa kujiendesha mfano kununua dawa, hizo meli, kuwezesha elimuu nk. Ili pesa hizo zipatikane inabidi tuuze nje mali zetu mfano, madini, mazao ya mashamba na kuwaleta watalii wengi zaidi ili watupe pesa za Kigeni. Hizo pesa za Kigeni ndizo zitumikazo kuagiza dawa na hizo meli na mafuta. Lakini, nchi yoyote inaweza kushindwa kuuza bidhaa zake ikiwemo mazao ya mkulima, Kim nyanya, maembe, pilipili, mihogo nje ya nchi hata km mazao hayo yamelimwa kwa wingi nchini, endapo nchi haina ndege zake. Ndio maana vitunguu vya Karatu vinanunuliwa kwa wingi na nchi jirani zenye ndege. Ila vinapouzwa nje ya nchi kupitia hao wanunuzi wa jirani, kule ulaya haviendi na nembo ya TZ, bali ya nchi jirani, na pesa za Kigeni pia huenda huko huko jirani na si TZ. Ili tuzipate pesa hizo, ni lazima tuwe na ndege za uhakika na za kutosha kiasi cha kushawishi mikataba ya soko nje. Soko likipatikana wakulima vijijini vipato vyao vitaongezeka, taifa litakuwa na kipato kikubwa, kisha litanunua meli nyingi tu na litaongeza ndege zaidi ili kuleta watalii wengi zaidi na ajira nyingi zaidi. After all usafiri wa anga ni businesses pia inayoigiza pesa za Kigeni za kununulia hizo meli na dawa. Subira na ushirikiano katika kipindi hiki cha mpito ni muhimu. Well done TZ kwa kuongezeka Ndege. Ni matarajio ya waitakiao TZ baraka za kiuchumi na maendeleo kuwa ndege nyingine itakuja soon.
ReplyDelete