Kutokana na hukumu hiyo, Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko amesema kuwa watalipa faini.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema kuwa katika ushahidi wa kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 3, huku utetezi ukiwa na shahidi 1.
Hakimu Mashauri amesema kuwa ameridhishwa pasina kuacha shaka juu ya ushahidi wa upande wa mashtaka hasa kwa uthibitisho uliotolewa na Mkemia Mkuu wa serikali kwamba mkojo wa mshtakiwa ulikutwa na chembe chembe za dawa za kulevya.
“Kutokana na kujiridhisha na ushahidi huo, namtia hatiani mshtakiwa kwa makosa hayo ya kutumia dawa za kulevya,”-Hakimu Mashauri
Baada ya Masogange kutoa utetezi wake, Hakimu Mashauri amesema kuwa ameusikia utetezi wa mshtakiwa kwamba apewe adhabu ndogo, huku upande wa mashtaka ukitaka apewe adhabu kali.
“Nimesikiliza maelezo ya pande zote, katika kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin namuhukumu mshtakiwa kulipa faini ya Sh.Mil 1 ama jela miaka 2.
” Katika kosa la pili la kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam, nakuhukumh kulipa faini ya Sh.Laki 5 ama jela miezi 12,” amesema Hakimu Mashauri.