Bunge lajadili sababu za kukatika Umeme

Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Nishati imesema na kudai kuwa kukatika kwa umeme mara kwa mara kunatokana na sababu nyingi na wala sio kutokuwepo kwa umeme au miundo mbinu pekee yake kama baadhi ya wananchi wanavyokuwa wanafikiria.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Medard Kalemani leo April kwenye kikao cha tisa mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linaendelea kufanyika Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge Temeke (CUF), Mh. Abdallah Mtolea aliyetaka kujua sababu zinazopelekea kukatika kwa umeme jiji la Dar es Salaam kwa ujumla mara kwa mara.

“Kukatika kwa umeme kuna tokana na sababu nyingi, siyo kwa sababu ya kutokuwepo kwa umeme au miundombinu. Wakati mwingine ni kasoro ndogo ndogo, tunakiri kabisa zipo changamoto za maeneo machache za kukatika kwa umeme kwenye baadhi ya nyakati za muda. Tunachokiomba ni kutupa taarifa inapotokea hitilafu ya namna hiyo”, amesema Dkt. Kalemani.

Dkt. Kalemani amesema katika majuma mawili yaliyopita palikuwepo na tatizo la umeme katika maeneo ya Mbagala Jijini Dar es Salaam lakini kwa sasa wameimarisha tatizo hilo na suala la umeme katika maeneo hayo kuwa vizuri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad