Bwege‘’ Akanusha Bungeni, Asapoti Waraka Wa Maskofu .

Bwege‘’ Akanusha Bungeni, Asapoti Waraka Wa Maskofu .
MBUNGE wa Kilwa Kusini, Said Bungara (CUF) maarufu kama ‘Bwege’, amesema hakubaliani na kipengele kilichopo kwenye hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kinachoeleza kuwa nchi yetu ina amani sana.



Bungara amesema hakubaliani na kipengele hicho kutokana na matukio mawili yaliyotokea jimboni kwake; tukio la msikiti kuvamiwa na mtu mmoja kupoteza maisha na mwingine kubaki na ulemavu wa macho, huku tukio lingine ni la vijana kuchukuliwa katika mazingira ya kutatanisha na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi ambapo mpaka leo watu wawili hawajajulikana walipo.



“Kuna Noah nyeusi ilikuja Kilwa na kukamata vijana wawili, usiku wake wakakamatwa vijana tisa, hatukujua wamepelekwa wapi, tulifuatilia mpaka Kituo cha Polisi Kilwa Masoko wakasema kweli wapo wameshikiliwa, nikamwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani (Mwigulu Nchemba), tisa kati yao waliachiwa, lakini wawili hawajarudi mpaka sasa na hatujui wako wapi. Nataka leo, waziri atupatie vijana wetu hao na ushahidi upo.



“Leo mnapotwambia nchi hii ina amani mimi siwaelewi, watu wamepigwa risasi msikitini, mmoja amekufa, mwingine ametobolewa jicho na mwingine kachomwa moto ndevu, hawa watu wapo na serikali haikutoa tamko lolote. Hii nchi imeharibika. Ninaunga mkono waraka wa maaskofu kwa sababu maneno ya maaskofu ni maneno ya Mungu, tunataka amani na utulivu,” amesema Bwege.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad