Staa wa muziki kutokea Marekani Ciara amemfungulia mashtaka mzazi mwenzake Future baada ya kusemekana kuwa hatimizi ahadi zake za kumuona mtoto wao Future Zahir Willburn mwenye umri wa miaka mitatu na kila ifikapo siku za kumuona basi huvunja siku hiyo kwa majukumu mengine binafsi.
Kupitia chombo cha habari cha TMZ kinadai kuwa Ciara amefungua mashtaka na kudai kuwa asilimia 37 ya muda wa Future haonekani kuwa karibu au kuja kumuona mwanae Furture Zahir na hata mtoto akijaribu kumtembelea baba yake anaishia kushinda nyumbani na bibi yake bila kupata muda na baba yake.
Rappa Future pamoja na Ciara walifanikiwa kuwa katika mahusiano ya kiampenzi kwa muda mrefu na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kiume Future Zahir na kuachana August 2014.