Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia vizuri mamlaka yake.
Kauli hiyo ya Fred imekuja baada ya mwanamke mmoja mkazi wa Kigamboni, Fatuma Lowassa (31), kujitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, jana Jumanne Aprili 10, akidai kutelekezwa na baba yake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Akiwa Monduli mkoani Arusha, Fred ametoa tamko akisema; “Nimesikia mwanamama mmoja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam.
“Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha.
“Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.” Ameandika Fred.
Mwanamke huyo amejitokeza jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni mwendelezo wa Makonda kuonana na wanawake waliotelekezwa na watoto na waume zao.
Mwanamke huyo amesema yuko tayari kupima kipimo cha DNA na Lowasa kuthibitisha kama kweli ni baba yake huku akijinasibu kumtafuta baba yake huyo kwa muda mrefu bila mafanikio.
“Nilipeleka barua Ikulu kuomba kuonana na baba kipindi akiwa Waziri Mkuu lakini niliitwa mimi na mama katika Klabu ya Mamba iliyopo Kinondoni, alikuja mwanamume akiwa kwenye gari lenye ‘tinted’ akatuhoji mimi na mama akaondoka hakutupa majibu yoyote hadi leo,” amesema Fatuma.
Aidha, amesema aliwahi kukutana na Fred na akamuahidi kumsaidia lakini hadi sasa amekuwa kimya
VIDEO:
SOMA PIA:Job Opportunity at East African Community, Internal Auditor
Ama kweli we mtoto, mambo ya wazee huyajui, hiyo issue mwachie Mzee anajua ukweli ulivyo, ushauri wa bure.
ReplyDeleteFred kauli yako ina utata. Km watu wa Monduli mnathamini watoto km ulivyodai, ni jambo jepesi tu kupima DNA, ili kubaini km huyu binti ni damu ya baba yako, kisha ikibainika ni wa familia yenu, basi mpe hiyo thamani ya wamonduli uliyoisema mnazo dhidi ya watoto. Wala usimkasirikie huyu binti, mama yake, makonda, taasisi iliyounda timu ya kusaidia watoto wengi ambao hali zao kimaisha zimekuwa duni kwa sababu ya kutelekezwa na wawazi wao. Lakini si wewe pekee, wengi wanapata shida kuamini kuwa mmoja wa wazazi wake aliwahi au anaweza kuwa na mahusiano nje ya maadili. Kumbuka baba yako ni binadamu, na hakuna binadamu aziyekosa. Ila mbaya, ni kuendeleza makosa badala ya kurekebisha. Mimba labda iliingia kimakosa, basi rekebisha kosa kwa kutoa huduma bora.
ReplyDelete