Derby Hazijaisha, Leo ni Vita ya Nafasi ya Pili Pale Madrid

Baada ya jana kushuhudia derby kali zadi katika msimu wa ligi kati ya Manchester City vs Manchester United, hii leo tunakwenda kuona derby nyingine ambapo Real Madrid wataikaribisha Athletico Madrid.

Tofauti na derby kati ya Man City na Man United, derby ya Madrid haina bingwa na wote hawa wawili wanapambana kwa ajili ya kutafuta nafasi ya pili katika msimu huu wa La Liga.

Athletico Madrid hawajawahi shinda hapa Bernabeu tangu 1999, lakini Athletico wamewahi kushinda michezo mitatu kati ya michezo 11 ambayo wamecheza katika uwanja huu wa Santiago Bernabeu

Katika michezo yao 4 iliyopita katika ligi, Athletico Madrid wamepoteza michezo miwili lakini ushindi wa 2-0 dhidi ya Sportinh katikati ya wiki unawapa hamasa kubwa kuweza kushinda mchezo wao wa leo.

Pamoja na kuuanza msimu kwa kusuasua, sasa vijana wa Zinedine Zidane wanaonekana kukaa vizuri katika La Liga, michezo yao 14 iliyopita, Real Madrid wamefanikiwa kushinda michezo 12.

Kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa kiasi fulani itaweka ajira ya Zinedine Zidane sehemu nzuri, ushindi wa leo utawapa alama 66 ikiwa ni alama 1 nyuma ya Athletico Madrid walioko nafasi ya pili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad