Najaribu kutafakari mwenendo wa Siasa za matusi na kejeli,mwenendo wa Siasa za kutishana na Mwenendo wa siasa zisizokuwa na amani kabisa uhuru kuminywa bila sababu za msingi.Wakati nawaza haya pia nahisi tupo wengi ambao tushafikiria haya.
Kati ya vitu ambavyo Wananchi huamini zaidi basi ni Dini pengine kuliko hata kingine chochote kile.Wananchi huamini viongozi wa dini kuliko wa vyama vya siasa au wanasiasa kabisa hii ni kutokana na uwoga juu ya nguvu zisizokuwa na kikomo kabisa (MUNGU)
Kiungo ambacho kinatumiwa kuunganisha watu wa rika zote,wa dini tofauti na daraja tofauti basi ni Dini.Dini ndo inawafanya watu wawe wamoja na kuzika tofauti zingine kwa sababu wote ni zao la Adam lkn leo kunatumika tofauti kabisa
Dini imeingiliwa na Siasa zisizokuwa na ukweli ndani yake.Siasa za chuki lengo kubwa ni kuwa nani achukue kundi kubwa la watu mwingine akose.Maaskofu wanaonekana wazalendo huku waislamu chini ya BAKWATA wanaoenakana kuunga mkono chama Tawala wala sio Wazalendo.Umeona shida hiyo?Tofauti za waziwazi kabisa.
Dini daima kama sehemu nyeti ya kulinda amani basi haifai kuingiliwa na Siasa kwa namna moja au nyingine.Inafaa iwe ni sehemu inayojitegemea peke yake wala haifai kuingiliwa
Tunaona Syria , Afghanistan,Iraq jinsi mambo yalivyowageukia kisa uingiliwaji wa Siasa na dini.Hata vita vya Eslael na Palestina ni hii ni kutokana na sintofahamu za Kidini ya Siasa kwa pamoja.Ni sababu zipi zinapelekea haya? Kwann yatokee?
Nawatakia Wakristo wote Pasaka Njema
Si useme tu kuwa kanisa limekuwa tawi la siasa la Chadema.
ReplyDelete