DRC Yasusia Mkutano wa Umoja wa Mataifa

DRC yasusia mkutano wa Umoja wa mataifa
Umoja wa mataifa hii leo unafanya mkutano maalum mjini Geneva Uswizi kuchangisha fedha za kukabiliana na janga la kibinaadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mashirika ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 5 wamelazimika kuyatoroka makaazi yao kwasababu ya mapigano katika sehemu tofauti ya nchi hiyo kubwa.

Lakini serikali ya DRC imekataa kuhudhuria mkutano huo wa ufadhili ikisema kwamba hali inafanywa kuwa mbaya wakati ni kinyume cha hicho.

Mkutano huo umedhamiriwa kuchangisha dola bilioni 1.7 kupunguza uzito wa inachotajwa na Umoja wamataifa kuwa ni janga kubwa la binaadamu nchini Congo.

Mpaka sasa serikali ya DRC haijajibu mualiko wa Umoja wa mataifa ikisema taasisi hiyo kuu imetilia chumvi hali halisi nchini na ukubwa wa tatizo lililopo.

Mashirika ya misaada yanasema watu milioni tano wamelazimika kuyatoroka makaazi yao kutokana na ghasia, mapigano, njaa na ukosefu wa utulivu na kwamba maelfu ya raia wa Congo wamelazimika kutafuta hifadhi magharibi mwa Uganda.

Wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu ndani ya DRC wamezusha wasiwasi kutokana na hatua hiyo ya serikali kususia mkutano huo mkuu mjini Geneva.

Wasiwasi wa aina hiyo pia umetolewa na baadhi ya raia wanoasema kwamba wataendelea kuteseka bila ya msaada wa kimataifa.

Je kuna hasara gani wa kwa serikali hiyo kukataa kuhudhuria mkutano wa Geneva?

Mashirika ya misaada yanasema DRC inateseka katika janga kubwa lenye uzito la kibinaadamu lililosahaulika kwa muda mrefu.

Kuna watu milioni 13 wanaohitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2 wanaugua utapia mlo mbaya, na watu milioni 4.5 wamepoteza makaazi yao.

Maafisa hatahivyo wa Umoja wamataifa wanatumai kwamba wanadiplomasia wa Congo watabadili uamuzi wao na wahudhurie mkutano huo leo.

Ni wazi kwamba mkutano wenyewe utaendelea licha ya chochote kile kitachotokea, wanaharakati wanasema maisha ya mamilioni ya watu yamo hatarini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad