Fatuma Karume: Sina Mpango wa Kuingia Kwenye Siasa

Fatuma Karume: Sina Mpango wa Kuingia Kwenye Siasa Mwanasheria maarufu nchini ambaye kwa sasa ndiye rais wa Tanganyika Law Society (TLS), Bi. Fatma Karu
me, amesema kwamba hana mpango wa kuingia kwenye siasa, licha ya kuonekana akikosoa sana wanasiasa na baadhi ya vitu vinavyofanywa na serikali.
Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Fatma Karume amesema hataki kuingia kwenye siasa kwa sababu anapenda kuwa huru, licha ya kwamba hatoacha kuendelea kukosoa serikali na wanasiasa pale wanapokosea.
“I like my freedom, napenda kufanya vile ninavyoona mimi, kama serikali inafanya vitu kinyume na sheria nitasema kwamba hivi sio vizuri, si vizuri kuvunjia watu majumba yao wakati kuna court order, nitasema sitaogopa, ila sitaki kugombea, sitaki siasa, I like to be left alone”, amesema Fatma Karume.
Fatma Karume ameendelea kusema kwamba kitendo cha kuonekana kuikosoa serikali mara kwa mara na kutetea baadhi ya vyama vya siasa, anafanya hivyo kwa sababu haungi mkono uvunjaji wa sheria kwa namna yoyote ile, iwe inafanywa na serikali au vyama vya siasa.
"Siungi mkono uvunjaji wa sheria hata ukiwa upande wowote, mimi ni mtu huru, kama kitu hakiendi kwa mujibu wa sheria nitasema, sio kwamba unakosoa vitu una ugomvi wa serikali, sijali", amesema Fatma Karume.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad