Mwanasheria maarufu nchini ambaye kwa sasa ndiye rais wa Tanganyika Law
Society (TLS), Bi. Fatma Karu
me, amesema kwamba hana mpango wa kuingia
kwenye siasa, licha ya kuonekana akikosoa sana wanasiasa na baadhi ya
vitu vinavyofanywa na serikali.
Akizungumza
kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Fatma
Karume amesema hataki kuingia kwenye siasa kwa sababu anapenda kuwa
huru, licha ya kwamba hatoacha kuendelea kukosoa serikali na wanasiasa
pale wanapokosea.
“I like my freedom, napenda kufanya vile ninavyoona mimi, kama serikali inafanya vitu kinyume na sheria nitasema kwamba hivi sio vizuri, si vizuri kuvunjia watu majumba yao wakati kuna court order, nitasema sitaogopa, ila sitaki kugombea, sitaki siasa, I like to be left alone”, amesema Fatma Karume.
Fatma Karume ameendelea kusema kwamba kitendo cha kuonekana kuikosoa serikali mara kwa mara na kutetea baadhi ya vyama vya siasa, anafanya hivyo kwa sababu haungi mkono uvunjaji wa sheria kwa namna yoyote ile, iwe inafanywa na serikali au vyama vya siasa.
"Siungi mkono uvunjaji wa sheria hata ukiwa upande wowote, mimi ni mtu huru, kama kitu hakiendi kwa mujibu wa sheria nitasema, sio kwamba unakosoa vitu una ugomvi wa serikali, sijali", amesema Fatma Karume.