Manara ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, 2018 kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa EATV baada ya kuwepo tetesi kuwa katika mchakato wa kumpata mmiliki wa timu kupitia upate wa hisa palikuwepo na uchakachuaji wa hali ya juu jambo ambalo walishindwa kuwapa fursa watu wengine.
"Nipo tayari kujiuzulu wadhifa wangu kama atatoweza kujitokeza mtu yeyote na kusema yeye alikuwa miongoni mwa watu waliotuma maombi ya kutaka kuiongoza timu zaidi ya Mohamed Dewji", amesema Manara.
Pamoja na hayo, Manara amesema kwa sasa akili zao wamezikita katika ubingwa na wala sio katika masuala mengine.
"Tunataka kila mwana Simba awekeze nguvu yake kwenye ubingwa mwaka huu, kwa hiyo vipaumbele vyetu namba moja ni ubingwa, mbili ubingwa, tatu ubingwa na nne ni transformation", amesisitiza Manara.