Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee ameendeleza hoja kuhusu matumizi ya fedha ambazo hazijulikani zimetumikaje, kama ilivyobainishwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
-
Kupitia akaunti yake katika Mtandao wa JamiiForums, Mdee amemtaka Rais Magufuli na Serikali kwa ujumla kuacha kutumia vitisho na badala yake wajikite kwenye kutoa majibu sahihi kuhusiana na matumizi ya fedha hizo, ili kuondoa mkanganyiko uliopo kwa wananchi
-
Aidha, Mbunge huyo amehoji masuala mengine 8 yenye utata yaliyomo kwenye Ripoti hiyo ya CAG na kuwataka wananchi waamke kutoka kwenye usingizi wa pono unaoligharimu Taifa
-
Mwisho, Halima Mdee amemueleza Rais Magufuli kupitia hayo mambo 8, ajipime kama amefanikiwa kuinyoosha nchi au nchi imemnyoosha
Sasa hawa wapinzani ni vichwa maji au wamekosa hoja za msingi? Kwa ufanunuzi uliotolewa na wadau mbali mbali hadi CAG mwenyewe kuhusiana na suala la pesa zinazodaiwa kupotea zimemfanya kila mtanzania kuelewa hata yule mtu wa kawaida tu. Jitihada za wapinzani au sijui tuwaite wajingani kuihusisha serikali ya Magufuli na ufisadi ni jitihada za hovyo sizoweza kufanikiwa.
ReplyDeleteWapinzani hawajaenda shule na inaonesha hawaelewi masuala ya kiuchumi na mipangilio ya hesabu zake.
ReplyDelete