Leo April 4, 2018 stori inayoshika headlines za kimataifa ni kutoka Libya ambapo Mahakama ya Tripoli imefuta kesi ya mauaji iliyokua ikimkabili Saadi Gaddafi, mtoto wa tatu wa aliekua rais wa Libya, Muammar Gaddafi.
Saadi Kaddafi amefutiwa mashtaka yote dhidi yake katika kesi ya mwanamichezo Bachir al-Rayani ambaye alifariki dunia mwaka 2006 baada ya kupigwa kichwani. Bachir Rayani alifariki dunia baada ya malumbano katika nyumba inayomilikiwa na Saadi Gaddafi.
Mahakama hiyo imemuhukumu Saadi Gaddafi kifungo cha mwaka mmoja, kwa kosa la ulevi wakati wa kifo cha rafiki yake, Bachir al-Rayani, kilichotokea katika nyumba ya Saadi Gaddafi. Mahakama ya kaskazini ya Tripoli iliahirisha hukumu yake mara kadhaa, na hatimaye ilimsafisha katika kesi ya mwanamichezo huyo.