"Hatuwezi Tukawaacha Kuwapeleka Gerezani"- Mwigulu

"Hatuwezi tukawaacha kuwapeleka gerezani"- Mwigulu


Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema haipendi kuona wananchi wake wakiwa magerezani wamesongamana lakini imedai inafanya hivyo kutokana na makosa mbalimbali wanayoyafanya hivyo inakuwa ngumu kuwaacha wakiwa nje.


Hayo yameelezwa na Waziri wa wizara hiyo Mwigulu Nchemba leo (Aprili 09, 2018) katika Mkutano wa 11 wa kikao cha Bunge cha tano kilichofanyika katika mkoa wa Dodoma wakati akitoa ufafanuzi wa suala la wafungwa kusongamana magerezani jambo ambalo limeibua hisia za wabunge wengi wakiwa bungeni wakitoa maoni yao mbalimbali kuhusu wafungwa.

"Sio kila gereza lina msongamano, tuna baadhi ya magereza ambayo katika mikoa ile yenye kiwango cha uhalifu ni kidogo hata msongamano magerezani ni mdogo. Sisi kama serikali hatupendi watu kuwa magerezani lakini tunawapeleka kwasababu ya uhalifu wanaoufanya na hatuwezi tukawaacha wahalifu wakawa nje tu", amesema Mwigulu.

Pamoja na hayo, Waziri Mwigulu ameendelea kwa kusema "kama watu watafanya uhalifu ni kwamba wataendelea kupelekwa magerezani nasio vinginevyo".

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni Jeshi la Magereza katika kutekeleza jukumu lake la kuwapokea na kuwahifadhi wahalifu kisheria pia hutoa huduma ya chakula kwa wahalifu hao kupitia bajeti inayotengwa na serikali kila mwaka wa fedha, ambapo gharama ya chakula kwa mfungwa mmoja kwa siku ni Shilingi 1,342.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad