Heche Atoa Kauli Nzito Baada ya Kutishiwa Maisha

Heche Atoa Kauli Nzito Baada ya Kutishiwa Maisha
Mbunge wa Tarime vijijini John Heche amesema kuna njama zinaendelea za kutishia maisha yake baada ya kuonekana akiikosoa Serikali kufuatia kauli zake ikiwemo kuhusu ufisadi uliofanyika katika vitambulisho vya taifa vya NIDA .

“Kwa kifupi kuhusu njama zinazoendela za tishio juu ya maisha yangu, imekuwa kawaida sasa kwa taifa letu ukionekana unaikosoa Serikali pengine unaweza ukatengenezewa ajali au vyovyote vile” –John Heche

“Mtakumbuka February 2 nilizungumza kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye vitambulisho vya taifa na upandaji wa bei uliofanyika lakini pia nilizungumza kuhusu sakata la ufisadi katika Passport, baada ya kuyazungumza hayo nikaanza kupata vitisho na kuambiwa nimegusa sehemu ambayo wakubwa hawataki uguse” –John Heche
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad