Hii Ndio Hotel ya Kifahari Aliyofikia Zari Dubai Kujiliwaza Baada ya Kumtema Diamond...Gharama zake Hizi Hapa

Zari The Boss Lady ametua nchini Dubai kwa ajili ya kula bata na kufurahia wikiendi ikiwa ni siku chache zimepita tangu aliposaini dili la mamilioni ya fedha na kampuni moja ya nepi za watato hapa Bongo.

Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka picha kadhaa akionyesha akiwa ameongozana na watoto wake wawili akiwemo Raphael G na Lil Q.

Zari na familia yake hiyo wamefikia kwenye moja ya hoteli maarufu Dubai inayofahamika kama Dusit Residence Dubai Marina. Gharama za Kulala kwenye hoteli hiyo kwa usiku mmoja kwa bei ya chini ni takribani 385,000 hadi 1,010,000.

Hata hivyo inadaiwa kuwa ex huyo wa Diamond hivi karibuni atarudi tena Tanzania kwa ajili ya kusaini mkataba mwingine na kampuni ambayo bado haijafahamika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad