Mchezo huo ambapo wengi walikuwa wakiamini Man City wataondoka na ushindi baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika wakiwa wanaongoza magoli 2-0 kwa magoli yaliokuwa yamefungwa na Vincent Kompany dakika ya 25 na Ilkay Gundogan dakika ya 30 lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili.
Kipindi cha pili pamoja na Man United kuwa ugenini wanaonekana kuja na plan B iliyowafanya wapate ushindi wa magoli 3-2, magoli ya mapema ya Paul Pogba yaliofungwa dakika ya 53 na dakika ya 55 yanaonekana kuwatoa mchezoni Man City kwa kiasi flani kitu ambacho kiliwafanya Man United wapate goli la ushindi dakika ya 69 kupitia kwa beki wao Chris Smalling.