Hizi Hapa Hatua Tatu za Ukuaji wa Mahusiano Kufikia True Love


Katika hatua yoyote ile watu waliopo ya kimaisha wana majeraha ya nyuma y yametokana na malezi, mazingira ya kukuaji, mahusiano nk. Mtu anaposikia kupenda kimsingi ni ule msukumo wa kutaka kuponya majeraha yake. Msukumo huo huzingatia matamanio na hisia na vitu vya namna hiyo na si SABABU. Unachotaka ndo hicho hicho na si kingine na ndio maana tunapenda kwa msukumo tofauti kulingana na majeraha yetu. Unapopenda unapitia katika hatua 3 mpaka true love;

Hatua ya kwanza ni kuchunguza chemistry yenu. Wakati huu mapenzi yanakua moto moto, ukisiakia tu sauti ya mwenzio moyo unalipuka. Hii ni hatua muhimu sana ya kufurahi na mwenzako na kuponya majeraha yako na moyo wako unakwambia kuwa huyu ndiye. Lakini kipindi hiki hakidumu muda mrefu, mapenzi yanaanza kuchosha na mnaingia hatua ya pili ya romantic love. Wapenzi wengi sana huishia hapa.

Hatua ya pili kila mtu anatafta kujua nafasi yake kwa wenzake. Hisia zinafanana na za hatua ya kwanza lkn hapa kunakua na ile hali ya kuhisi umechokwa, uhitajiki, hupendwi km zamani, hujaliwi kihisia km inavyopasa. Hiki ni kipindi cha malalamiko, kilio, kuona mapungufu tu kwa mwenzio usione mazuri, frustration, kugombana sana na kupatana n.k. Hiki ni kipindi cha maumivu kwa wahusika wote wawili. Kipindi hiki ni cha mpito lakini wapenzi wengi huishia hapa kwa kutokujua umuhimu na faida yake. Wengi aidha wataachana au watapumzishana.

Hatua ya tatu ni TRUE LOVE. Baada ya mapambano makali ya nafsi zetu zilizojeruhiwa na za wapenzi wetu zilizojeruhiwa pia tunaamua ku "give up" na kukubaliana. Tunaamua kukua na kutengeneza mawasiliano mapya ya kuelewana, kujieleza, kueleza mioyo yetu, hofu, hisia. Tunatengeneza tabia mpya inayoendana na kila mmoja anaanza kumsapot mwenzie na si kujali tu matakwa yake. Mabadiliko makubwa hutokea, hali ya kujihami huisha na kila mtu hiweza kumtimiliza mwenzake. Katika hatua hii tunasikia ubongo umerelax, kinga ya mwili imeimarika, n' relaxing of the nevous system. Tutagobana na kusuguana na bado tutakutana na changamoto ktk hatua hii lkn tumekubaoiana kukabiliana nazo kwa mustakabali wa maisha yetu. So TRUE LOVE haitokei tu km bahati
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad