Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa kwa kuzingatia kiapo chao wataendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Dk. John Pombe Magufuli katika jitihada za kuleta maendeleo.
Akizungumza leo wakati Rais Magufuli azinduzi wa ukuta wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara, Mobeyo amesema kuwa uhodari wao ndio nguzo kubwa ya Jeshi hilo.
“Tutazingatia kiapo chetu, uaminifu wetu, utii wetu na uhodari ambayo ndio nguzo kubwa kwa jeshi letu, tutaendelea kukuunga mkono katika jitihada zako za kuliletea maendeleo Taifa letu Mh. Rais na Amiri Jeshi Mkuu sisi tuko tayari kwa Watanzania wenzangu nawasihi sana tujivunie Tanzania yetu na tuilinde jukumu la ulinzi wa Taifa letu ni letu sote na jukumu la kuleta maendeleo kwenye Taifa hili ni la Watanzania wote,” amesema Mobeyo.
“Tuutunze ukuta huu na ibakie kuwa alama ya umoja wetu kulinda rasilimali zetu tufanye kazi kwa manufaa ya Taifa letu , Tanzania ndio Tunu tuliopewa na Mwenyezi Mungu tuilinde amani yetu na kuidumisha kwa gharama yoyote ile, Jeshi la Wananchi wa Tanzania liko imara kwa umoja wetu tutafanikiwa,” ameongeza.