Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linawashikilia watu saba wakidaiwa kuhamasisha maandamano yanayodaiwa kufanyika April 26 mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha , Kamishina msaidizi mwandamizi, Yusuph Ilembo amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakihamasha maandamano kupitia mitandao ya kijamii ikiwapo Telegram na WhatsApp.
Amesema watu watatu kati ya hao saba ni wanafunzi wa vyuo vikuu na walitiwa nguvuni na jeshi hilo mara baada ya kufanya upelelezi wa kiitelejensia na kubaini ushawishi waliyokuwa wanaufanya kupitia mitandao hiyo.
“Nasisitiza hakuna maandamno Aprili 26, atayeandamana atavuna alichopanda kwa serikali hajaribiwi,” amesema Ilembo.
Baadhi ya watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote, huku wakiendelea kuwatafuta wengine kwa njia mbalimbali.