Mara nyingi ipo migogoro mingi inayotikea katika mahusiano ya kimapenzi, na mitafaruko hiyo hupelekea ndoa hizo kufa kabisa, hivyoili uweze kuepuka mitafaruko hiyo unatakiwa kufanya yafutayo;
1. Uwe mwangalifu, katika mahusiano yako kwa kuangalia kipi cha kusema na kipi si cha kusema.
Unapkuwa katika mahusiano na umegombana na mwenza wako tafadharu sana chunga sana kinywa chako kwa sababau kinywa chenye maneno yenye hekima huleta maelewano ndani ya nyumba, na pia kinywa kichafu husababisha ugomvi katika mahusiano.
Hivyo basi ili kuleta maelewano na mwenza ambaye mmegombana hakikisha unachunga sana maneno yatokayo katika kinywa chako. Kwa sababu unapotamka maneno makali maneno mengine huamsha molali wa ugomvi kutoka kwa mwenza wako.
2. Jambo la pili ni kuhakikisha unashusha sauti wakati unazungumza na mwenza wako.
Najua fika ugomvi husababisha sauti yenye mpayuko wa sauti za juu, hivyo ili kupunguza mitafaruko na mwenza wako mliyogambana ili kufikia maridhiano na mwenza wako mliyegombana hakikisha ya kwamba unakuwa katika hali ya kuzungumza kwa sauti ya chini, kufanya hivi kutakupa hali ya unyenyekuvu mbele ya nafsi yako na mwezi wako.
Hivyo kama unataka maridhiano katika ndoa yako hakikisha unayazingatia hayo.
Kwa leo sina la ziada nikusihi endelea kusoma habari na makala mbalimbali kutoka hapa Muungwana Blog. Asante