John Heche Afunguka Mazito Baada ya Mdogo Wake Kuuwawa Kikatili na Polisi

John Heche Afunguka Mazito Baada ya Mdogo Wake Kuuwawa Kikatili na Polisi
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefunguka kuwa mpaka sasa haelewi ni kwa vipi mtu anaweza kuuwawa na polisi kwa kuchomwa kisu tena akiwa amefungwa pingu huku akikumbushia tukio la mdogo wake mwingine kujeruhiwa vibaya na polisi ambapo alisababishiwa ulemavu mwaka jana.


Mbunge Heche amesema kwamba mtu kuchomwa kisu mgongoni ni kudhamiria kuua kwasababu mtu huyo hakuwa anapambana.

"Nilijua mikononi mwa polisi ni sehemu salama, wiki mbili zilizopita kijana Allen alikufa katika mazingira tata kule Mbeya, Mwanza mama aliyekamatwa na kunyimwa dhamana mtoto wake mchanga alikufa. Leo ni kwangu mdogo wangu ameuwawa kikatili sana mikononi mwa polisi. Maisha yangu yote nimeyatoa kupigania haki ili watu wasionewe, mtuhumiwa asifanywe mkosaji na kuhukumiwa kabla ya vyombo vya sheria kumhukumu,"  Heche.

Ameongeza " Mwaka jana mdogo wangu mwingine aliumizwa vibaya sana na polisi. IGP Mangu na RPC waliokuwa Tarime walilipa uzito suala hilo lakini walipoondolewa, suala liligeuzwa kisiasa na wale vijana waliokua wamemjeruhi mdogo wangu ambaye mpaka sasa sikio moja halisikii,wakarudishwa kazini kinyemera na kuhamishwa Tarime kama kunikomoa. Mimi nimewahi kutishiwa kuuwawa kituo cha polisi, najisikia maumivu makubwa mno lazima Watanzania wakatae hali hii".

Pamoja na hayo Mbunge huyo amehoji juu ya ukimya wa Waziri na kuongeza kwamba ni watu wangapi wanakufa na kuumizwa mikononi mwa polisi bila matukio kujulikana wala kutangazwa na kuweka wazi kwamba atazungumza muda ukifika.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad