Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 24, bungeni mjini Dodoma, Heche amesema licha ya kutotishika na vitisho hivyo amebainisha kuwa kuna kesi inaandaliwa dhidi yake na muda wowote anaweza kukamatwa.
“Kuna njama za kutishia watu wanaohoji masuala mbalimbali ambayo tunayazungumza na kuonekana wazi kuigusa Serikali,” amesema.
Sakata la mradi huo lilitikisa katika mkutano wa Bunge uliofanyika Februari mwaka huu, ambapo mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde pia aliligusia na kubainisha kuwa mradi huo umekuwa ikitekelezwa kwa gharama za Dola 40milioni za Marekani, wakati taarifa zilizopo ni kuwa mradi huo ulikuwa na thamani ya dola 16 milioni za Marekani, sawa na Paundi 11 milioni.
Mradi huo wa hati za kusafiria ulizinduliwa Januari 30, 2018 na Rais John Magufuli.