Mh. Shonza ameyasema hayo wakati akjibu swali la mbunge wa Singida Mjini Mussa Ramashani Sima ambaye alihoji kuhusu mamlaka ya Waziri katika kusimamia kazi za TFF ikiwemo mapato na matumizi ya shirikisho hilo kutokana na katiba ya TFF kutoruhusu kuingiliwa na serikali.
''TFF pamoja na viongozi wake wote, wanapaswa wanalazimika na hivyo wanatambua mamlaka ya Waziri, kwasababu katiba ya TFF inatambua kuwa TFF ni chombo cha mpira ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya Baraza la Michezo ya 1967 na marekebisho yake ya mwaka 1971'', amesema Shonza.
Aidha Mbunge Mussa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Singida amemuomba Waziri kuhakikisha wanaibana TFF ili ipeleka mpango kazi kwenye vyama vya mikoa ili kujua matumizi ya pesa za ruzuku zinazotolewa kwa shirikisho hilo.