Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz jana Jumatatu Aprili 16 alishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano kufuatia kusambaza picha zisizo na maadili.
Mambosasa ameiambia MCL Digital leo Jumanne Aprili 17 kuwa Diamond alihojiwa na kupewa dhamana jana Jumatatu huku uchunguzi zaidi ukiwa unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi.
“Alihojiwa jana na akapewa dhamana, upelelezi unaendelea,” amesema Mambosasa.
Leo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema polisi inamshikilia msanii huyo na Nandy ambao kwa nyakati tofauti wanadaiwa kusambaza picha sisizo na maadili kwenye mtandao.
Wasanii hao wanadaiwa kusambaza picha hizo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.
Serikali na taasisi zake wanatakiwa kuwa na nguvu zaidi ya teknolojia katika kupambana na makosa ya kimtandao kuliko ilivyo hivi sasa. Ajabu Tanzania tuna uhusiano mzuri sana na China kwanini tusitumie urafiki wetu huo tukapata msaada wa taaluma ya kuthibiti makosa ya kimtandao kwani Wachina wapo vizuri sana katika nyanja hiyo. Kutokana na uzito na umuhimu wa masuala ya kimtandao nchi nyingi Duniani sasa zimeunda batalioni mpya katika vikosi vyao vya jeshi badala ya vikosi anga,vukosi vya nchi kavu,vikosi vya majini na sasa kikosi cha mtandao nk. Ulinzi katika Masuala ya mtandao kwa nchi za wenzetu sio masuala ya polisi tena bali ni masuala ya kijeshi. Tungeomba seriaki yetu kulipa uzito suala hili kwani Dunia inabadika kwa haraka sana. Na upande mwengine kutafungua hata nafasi za ajira kwa vijana wetu.
ReplyDelete