Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema Akamatwa na Polisi Kisa Maandamano ya Mange Kimambi

Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema  Akamatwa na Polisi Kisa Maandamano ya Mange Kimambi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limedhibitisha kumkamata Katibu wa Baraza la Wanawake la Chadema, Elizabeth Mambosho.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Aprili 26 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro amesema wamemkamata na kumuhoji kwa kosa la kuhamasisha maandamano kwa njia ya mtandao.

"Ni kweli tulimkamata jana usiku na kumuhoji kwa kosa la kuhamasisha maandamano kwa njia ya mtandao na tumemwachia kwa dhamana," amesema Muliro.

Amesema kuwa wanaendelea na upelelezi utakapokamilika akibainika anakosa watamfikisha mahakamani kujibu tuhuma.

Kuhusu polisi kuzagaa mtaani amesema Jeshi la Polisi lina utaratibu wa kuimarisha ulinzi kila kunapokuwa na sikukuu za kidini na zile za kiserikali.



"Ni kweli polisi wetu wako kwenye doria maeneo yote ni utaratibu wetu kila kunapokuwa na sikukuu za kidini na zile za kiserikali hivyo watu wasiwe na wasiwasi waendelee na shughuli zao kama kawaida," amesema Muliro.



Amewataka wakazi wote kuachana na uvunjifu wa sheria hasa kwa njia ya mtandao kwani jeshi liko imara kupambana na wahalifu watakaojaribu kuvunja sheria.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad