Katika Kumuenzi Sokoine Watanzania Tuige Mfano Wake- Rais Magufuli

Katika Kumuenzi Sokoine Watanzania Tuige Mfano Wake- Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwataka watanzania kumuiga hayati Edward Moringe Sokoine ambaye alikuwa Waziri wa pili wa Tanzania aliyefariki April 12, 1984.


Rais Magufuli amesema hayo leo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 34, Sokoine ambaye alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam na ilikuwa ni siku ya Jumatano.

"Katika siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehemu Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi shujaa huyu niliyemjua na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho. Wakati tunapoadhimisha siku kama hii ya kifo chake, watanzania tuige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa, ufisadi, unyonyaji, mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa"

Aidha Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kumuenzi kwa kujenga umoja na kupiga vita rushwa kama ambavyo alikuwa akifanya enzi za uhai wake.

"Marehemu Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wangu kwa watanzania tumuige na kumuishi. Ni rai yangu pia tumuenzi kwa kujenga umoja wetu , kupiga vita rushwa na kuchapa kazi Mungu aiweke roho ya marehemu Edward Moringe Sokoine mahala pema peponi" alisema Magufuli
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad