Kauli ya Mzee Akilimali Baada ya Kufuzu Hatua ya Makundi CAF

Kauli ya Mzee Akilimali Baada ya Kufuzu Hatua ya Makundi CAF
Baada ya kusonga mbele mpaka hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Mjumbe Mkongwe wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, ametoa pongezi kwa klabu yake.

Akilimali amewasifu vijana wake kwa namna walivyopambana kuhakikisha wanafuzu kuingia hatua hiyo kutokana na kuiondosha Wolaita Dicha SC.

Mjumbe huyo ameelezea furaha yake kwa wachezaji wa kikosi hicho huku akisema bado wanahitaji kushikwa mkono ili wajitume zaidi haswa kuelekea mechi zingine zitakazofuata.

Kikosi hicho kimewasili usiku wa leo jijini Dar es Salaam na kupokelewa na baadhi ya mashabiki katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Yanga imefuzu kuingia hatua hiyo kwa idadi ya mabao 2-1, ambapo katika mechi ya mkondo wa pili ilikubali kufungwa bao 1-0 Aprili 18 wiki hii huko Awassa, Ethiopia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad