Jana Aprili 14, 2018 Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilipata
Rais mpya mteule Bi. Fatma Karume, Hatimaye Mhe. Tundu Lissu ambaye
ndiye aliyemuachia kiti hicho ametoa pongezi kwa wana
Mhe. Lissu ambaye yupo hospitalini nchini Ubelgiji tangu mwezi
Januari mwaka huu, amesema kuwa uchaguzi huo umethibitisha kuwa TLS ni
chama ambacho kinaweza kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa na
mtu.
“Napenda kuwapongeza wanachama wote wa Chama cha Mawakili
Tanganyika (TLS) kwa kumchagua Bi. Fatma Karume kuwa Rais mpya wa TLS.
Uchaguzi huu umethibitisha, kwa mara nyingine tena, umuhimu wa Chama cha
kitaaluma cha mawakili kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa,“ameeleza Tundu Lissu na kutoa pongezi kwa Bi. Fatma .
“Namtakia Rais Mteule Fatma Karume kila kheri katika
kutelekeza majukumu yake mapya na muhimu katika kipindi hiki cha
historia ya nchi yetu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Wakili Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS) jana mjini Arusha kwa ushindi wa kura 820
akiwamwaga Godwin Ngwilimi kura 363, Godwin Mwapongo 12 na Godfrey
Wasonga kura 6.