Mbunge wa jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amefunguka kuhusu kitendo cha mdogo wa Mbunge Heche wa Tarime aliyeuawa na polisi aliyetajwa kwa jina la William Marwa kuwa kimemsikitisha sana.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ridhiwani ameandika “Kitendo kilichotokea sio tu kimesikitisha ukoo wa Bwana Heche lakini kwangu binafsi. Jeshi letu limetengenezwa kulinda watu na mali zao sio kuumiza wasio na hatia“
“Ni imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya Heche. Poleni sana kwa msiba. Mungu awape subira John Heche” -Ridhiwani Kikwete
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amesema tayari wanamshilia askari wake mwenye namba E1156 Koplo William Marwa kwa tuhuma za kusababisha kifo cha kijana Suguta Chacha mwenye umri wa miaka 26.