Kimenuka Yanga Wataka Uchaguzi wa Viongozi Ufanyike

Kimenuka Yanga Wataka Uchaguzi wa Viongozi Ufanyike
Mara baada ya jana Yanga kupoteza mchezo wake kwa kufungwa bao 1-0 na wapinzani wao Simba SC, Uongozi wa Tawi la Umoja ya timu hiyo wameomba kufanyike uchaguzi wa haraka ili kuweza kuwa na viongozi ambao wataweza kuipeleka Yanga kufanya vizuri katika mashindano yaliyopo mbele yao.


Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Umoja la Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Waziri Jitu na kusema kwa sasa hawana viongozi kwa mujibu wa katiba na wanasikitishwa na hali halisi iliyo ndani ya klabu hiyo kwani hawana imani na viongozi waliomadarakani kwa sasa kwani hata matokeo ya jana Aprili 29, 2018 yamechangiwa na wao.

"Viongozi waliopo madarakani bado hawawezi kufanya uchaguzi, sasa sisi tunachoomba ni kwamba viongozi waliopo madarakani hapa huu ndio uwezo wao na wanayanga tutulie kwa sababu sisi tunadai uchaguzi na serikali wanajua kwamba Yanga haina viongozi kwa mujibu wa katiba yetu, tunadai uchaguzi", amesema Waziri Jitu.

Aidha, Jitu amewaomba wanachama kuendelea kutulia ili kutokuwachanganya wachezaji ambao wapo katika maandalizi mazito ya mashindano ya kimataifa kwa sasa.

Kwa upande mwingine, Jitu amesema endapo viongozi waliopo madarakani wangekubali kufanya uchaguzi mapema basi katika mechi ya jana wangekuwa na uwezo wa kuwafunga Simba kutokana na Mwenyekiti wanaomuhitaji kuwa na mapenzi ya dhati na klabu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad