Mjadala mkali unaendelea nchini Tanzania baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad kutoa taarifa yake ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mwaka 2016/17. Taarifa hiyo ilio wazi kwa umma, baada ya kukabidhiwa rasmi bungen imepokewa Kwa hisia tofauti huku baadhi wakihoji upotevu wa fedha za umma ambazo inasemekana huenda zimepotea.
Zitto Kabwe ambae ni mwanzilishi wa Chama cha ACT Wazalendo amezungumza na BBC kuhusu matokeo ya ripoti hiyo: