Liverpool Kupimana Nguvu na AS Roma Leo

Liverpool Kupimana Nguvu na AS Roma Leo 
Vita ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea tena usiku wa leo ambapo Liverpool wata


kuwa wanaikaribisha AS Roma kwenye Dimba la Anfield.

Liverpool waliingia hatua ya nusu fainali baada ya kuing'oa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1 huku nyota wake Mohamed Salah aking'aa.

AS Roma nao walitinga hatua hiyo kufuatia kupindua matokeo dhidi ya vinara wa ligi nchini Spain, FC. Barcelona.

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka duniani, itaanza majira ya saa 3 na dakika 45 za usiku.

Baada ta mtanange huo, kesho pia ligi hiyo itaendelea kesho kwa Bayern Munich kuikaribisha Real Madrid kutoka Spain.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad