Lulu Diva Ajikuta Akimwaga Chozi Hadharani Kisa Hiki Hapa

Lulu Diva Ajikuta Akimwaga Chozi Hadharani Kisa Hiki Hapa
MWANA-MUZIKI Lulu Abass ‘Lulu Diva’ hivi karibuni alidondosha chozi mbele ya wanafunzi wa Shule ya Lord Baden iliyopo Bunju jijini Dar alipokuwa amewatembelea na kilichomtoa machozi ni kumbukumbu za yeye kushindwa kusoma.



Lulu alimwaga machozi  alipokuwa akitoa wosia kwa wanafunzi hao kuhusiana na masomo kwani yeye hakupata nafasi ya kusoma kama wao licha ya kwamba alitamani kusoma ili aufanye muziki vizuri zaidi.



“Nikiwaona hivi mpo shule na mimi natamani sana nirudi shule kwa sababu muziki bila elimu ni shida, nyie mliopata nafasi hiyo mjitahidi sana kuzingatia masomo maana hakuna chochote kinafanyika bila elimu,” alisema Lulu Diva huku machozi yakimbubujika
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad