Buhari ameitwa na wabunge ili waweze kujadili hali ya usalama katika Jimbo la Benue. Pia wabunge hao Jumatano walipitisha kura ya kutokuwa na imani na wakuu wa masuala ya usalama.
Maaskofu wa Kikatoliki wanamshutumu rais kwa kupuuza wito wa mara kwa mara wa kumtaka kutupia macho tatizo la usalama wenye upogo na mbinu dhaifu za kudhibiti mapigano kati ya Wakristo ambao ni wakulima na Waislamu ambao ni wafugaji.
Hali hii ya kushindwa iwe ni kutokana na utendaji dhaifu au ukosefu wa utashi wa kisiasa, ni wakati wake sasa kuchagua njia ya heshima na kufikiria kujiuzulu kuliokoa taifa hilo ili lisididimie kabisa.
“Kwa kuwa rais ambaye anawateua wakuu wa usalama amekataa kuwaita na kuwapa amri, tunachoweza ni kuhitimisha kwamba wanatekeleza majukumu yaliyoandikwa ambayo yeye ameridhia,” imesomeka taarifa ya maaskofu hao.
Taarifa hiyo imekwenda mbali hadi kusema kwamba rais amepoteza kuaminika kwake kwa wananchi kutokana na kushindwa kwake kuiweka nchi kuwa salama.
“Kushindwa huku kuwa ni kutokana na uwezo wake mdogo kiutendaji au ukosefu wa utashi wa kisiasa, wakati umefika kwa yeye kuamua njia ya heshima na kufikiria kukaa kando ili kuliokoa taifa lisiangamie kabisa”.