Maaskofu wa KKKT Wasikitishwa na Wanaopinga Waraka Wao

Maaskofu wa KKKT Wasikitishwa na Wanaopinga Waraka Wao
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa wao kama Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamesikitishwa na watu ambao wanapinga waraka wao na kusema ni wajinga


Askofu Shoo ametoa kauli hiyo April 1,2018  katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini, mkoani Kilimanjaro na kusema kuwa wao wataendelea kusema ukweli siku zote

"Sisi tunasikitika sana tunaposema jambo la kweli, jambo linalohusu maisha ya watanzania wote katika waraka ule tuliotoa kama waraka wa maaskofu halafu kuna watu wachache wajinga mimi nimesema wamesema maaskofu wamesema sababu sadaka zimepungua kanisani, sisi sadaka haijapungua kwani wakristo wameendelea kujitoa sana na hatujapungukiwa na kitu napenda kuwashukuru na Mungu awabariki sana, na sisi tutaendelea kusema ukweli na wanaotaka kuharibu ukweli huo waendelee kuharibu lakini watanzania walio wengi, watanzania wenye hekima wanaelewa maneno tuliyozungumza siyo maneno ya kujibu tu haraka haraka bali maneno ya kututafakarisha"

Askofu Shoo aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo na kusema kuwa

"Tutaitwa majina mengi lakini tunajua ni jitihada za ule upotoshaji wa ule ukweli uliopo katika ule waraka, siyo jambo la hivi hivi tu kwa wakati mmoja maaskofu wa makanisa mawili makubwa hapa nchini kukaa na kutoa waraka, hatukukaa na kusema tutatoa waraka lakini Baraza la Maaskofu wa Katoliki wakakaa na kuja na ule waraka sisi wa KKKT tutakaa tukaja na waraka ukilinganisha ujumbe ni ule ule mimi nasema tena kuna kitu Mungu anataka kutuambia kama Watanzania kupitia ujumbe ule. Mungu awaguse hao wanaotumia nguvu nyingi kutaka kupotosha waraka ule, wanatumia nguvu nyingi kupaka matope"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad