Makosa Wanayofanya Wanandoa Wawapo Chumbani na Wenzi Wao
0
April 06, 2018
Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.
Leo ningependa kujadiliana na wewe msomaji wangu kuhusu makosa ambayo watu wengi huwa wanayafanya wawapo chumbani na wenzi wao, hususan wanandoa au wapenzi wanaoishi pamoja.
Wapenzi wengi wanaishi kwa mazoea, hawajui nini wafanye na nini wasifanye kwa ajili ya kupalilia mapenzi yao na matokeo yake, inakuwa rahisi mume kumchoka mke au mke kumchoka mume kwa sababu ya vitu ambavyo wahusika wenyewe ndiyo wamevikaribisha.
Yapo makosa ambayo watu wengi wamekuwa wakiyafanya wawapo chumbani na wenzi wao, iwe ni kwa kujua au kwa kutokujua.
Hakuna muda wa muhimu kwa wanandoa au wapenzi wanaoishi pamoja, kama ule muda kabla hamjapitiwa na usingizi. Ukiwa makini, utayafurahia mapenzi lakini ukikosa umakini na kuyafanya makosa yafuatayo, utakuwa unaiua ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe.
Yafuatayo ni makosa ambayo wapenzi wengi huyafanya kila siku na kusababisha mapenzi yapungue taratibu:
•KWENDA KULALA MUDA TOFAUTI
Yawezekana watu wengi wanalichukulia suala la kila mmoja kwenda kulala kwa wakati wake kama jambo la kawaida. Kwamba wanandoa au wapenzi wanaishi pamoja lakini kila mtu ana ratiba yake ya kwenda kulala, huyu akiwahi leo kupanda kitandani, yule anachelewa, yule akichelewa huyu anawahi, ilimradi tu mnapishana.
Wataalamu wa uhusiano wanaeleza suala hili kuwa sumu kali kwa wapendanao kwa sababu kisaikolojia, unapopanda peke yako kitandani kulala, nafsi inajihisi upweke na taratibu inaanza kujitenga na ya umpendaye.
Mkiendelea hivi kwa muda mrefu, hisia zinapungua na baadaye unaanza kumchukulia mwenzi wako kama mtu wa kawaida tu, ambaye hata asipokuwepo au ukikosa ukaribu wake maisha yako yanaendelea kama kawaida.
Kama na wewe ni miongoni mwa watu wenye tabia hii, badilika mara moja. Hutakiwi kuwa na visingizio katika hili, muda wa kulala ukifika, hakikisha unaambatana na mwenzi wako kupanda kitandani.
Faida nyingine ya kuongozana pamoja kwenda kulala, hata kama kulitokea mikwaruzano ya hapa na pale kutwa nzima, huu ndiyo muda mzuri ambao kila mmoja anaweza kueleza dukuduku lake na kumaliza tofauti kati yenu.
Tags