Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan, jana Jumanne, Aprili 10, amezindua chanjo ya kukinga saratani ya
mlango wa kizazi (HPV Vaccine), kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem
jijini Dar es Salaam.
Kinga hiyo itakuwa ni kwa wasichana kuanzia umri wa miaka 14 ambapo
amesema itatolewa bila malipo na kwa mwaka huu itatolewa kwa wasichana
616,734.