Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) ambapo anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mkutano huo ambao Kaulimbiu yake ni “Kuelekea Mustakabali wa Pamoja” unafanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mhe. Theresa May na umefunguliwa na Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza hapo jana April 19, 2018.
Majadiliano ya Mkutano wa CHOGM 2018 yatajikita kwenye maeneo manne makuu ya kipaumbele ambayo yatajadili namna Jumuiya ya Madola inaweza kufikia mustakabali wenye ustawi zaidi; mustakabali endelevu zaidi; mustakabali wenye haki zaidi; na mustakabali wenye usawa zaidi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano.
Mama Samia Kumuwakilisha Rais Magufuli kwenye Mkutano CHOGM
2
April 20, 2018
Tags
Licha ya sera za Magufuli za kuamua kujikita zaidi na masuala ya ndani ya nchi Kwanza na kutokuwa mtu wa kusafiri nchi za nje lakini maamuzi yake ya kuwakilishwa na mama SAMIA katika baadhi ya shughuli za nchi kimataifa ni moja ya kitu cha kujivunia sana sisi kama watanzania. Kitendo cha serikali ya awamu ya Tano cha kuwapa nafasi kina mama zetu kushiriki shughuli za kimaendeleo kikamilifu kwa kweli ni cha kufarahisha na kutia moyo sana. Tunaweza kuona ni vitu vidogo au hata wengine wakabeza lakini kama kuna kitu kimoja cha maendeleo cha kujivunia katika serikali ya awamu ya tano ya Tanzania basi ni ushirikishwaji wa akina mama katika kuiendesha nchi. Tumeona licha ya mama SAMIA, kuna mawaziri na Manaibu waziri na nyazifa nyenginezo nyingi katika upande wa wanawake kwenye serikali ya Magufuli ambao kwa mweli wanafanya kwa viwango vya kushangaza sana kutokana na ufanisi wao bora. Kama watanzania lazima tujivunie na mafanikio haya. Siku zote nasema na kwa sababu ni miongoni mwa watanzania niliobahatika kuwa na uweledi jinsi nchi za wenzetu wanavyoendesha shughuli zao za serikali. Na kwa kusema hivyo kwa kuwa maisha yangu mengi nimeyaishi na kuendelea kuishi katika nchi za ulimwengu wa kwanza yakwamba Nchi yetu ya Tanzania ina demokrasia tena sana lakini kama nchi nyingi za ulimwengu wa tatu tatizo umasikini jitihada zetu huwa hazionekani kuliko mapungufu yetu . Chukulia nchi kama Saudi Arabia ambayo ni rafiki wa karibu na kipenzi wa nchi za Magharibi na mshirika wao mkubwa. Sasa wale hawana mfumo wa vyama vyingi. Pale kamwe hakuna siku mtu asiekuwa Muislam kupata uongozi wa aina yeyote ndani ya serikali yao na sio muislam tu awe muislam wa madhehebu ya suni. Tuachane na China ambao tunajua ipo kivipi kisiasa lakini Marekani nao hawatokuwa tayari kuona nchi yao ikiongozwa na Muislam kamwe hicho kitu hakitatokea. Obama licha yakuwa na mlezi wa wake wa kiroho kwa miaka mingi na kanisa alilokuwa akisali likijulikana lakini wamerakani walihoji jina lake halikuwa vizuri walisema la kiislam kiislam hivi. Kwetu Tanzania hatubaguwi dini ya mtu, kabila la mtu au kipato chake linapokuja suala la uongozi na ndio maana tuna Raisi mkirsto makamo wake Muislam na ni mwanamama, nakadhalika nakadhalika.Na shughuli za nchi zianaendelea kiasi kwamba si rahisi kufahamu kama kuna utofauti wa imani miongoni mwa watanzania. Vitu kama hivi vingekuwa vinatokea katika nchi za wazungu basi sisi waafrica na watanzania tungelipewa masharti ya misaada ili kwenda kujifunza jinsi ya kuishi kama watanzania . Lakini kwa kuwa Tanzania ni nchi ya kiafrica na masikini mfumo wake wa kuheshimu haki kwa watu wote hauwezi kupigiwa mafano wanasubiri siku kuna machafuko ndio wanakuja kuelezea madhaifu peke yake. Sisi watanzania kama kuna kitu tunapaswa kukijutia sana hivi sasa na tutakuja kujuta zaidi hapo baade ni ile hali ya baadhi ya Watanzania kuamua kumpiga au kujaribu kumkwamisha Magufuli kwa kisingizio cha demokrasia? Tusidanganyane sisi watanzania hata tuwe na demokrasia ya aina gani kama bado masikini na tunashindwa kujitegemea sisi wenyewe kihali na mali basi bado ni watawaliwa tu. Kuikosoa serikali ni sawa kabisa kwani hata kama kungelikuwa na mfumo wa chama kimoja Tanzania basi wakosoaji wangekuwepo tu kwa nia ya kuhakikisha Serikali inajisahihisha katika kutenda kilichosawa kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake. Lakini ukosoaji tunaouona kutoka kwa baadhi ya upinzani Tanzania si ukosoaji bali ni upingaji. Ni upingaji kutoka vyama pinzani juu ya serikali ambao haulengi kuisadia serikali bali lengo lake ni kuikwamisha serikali katika kutekeleza na kufikia malengo ya maendeleo na huu ni upumbavu . Siamaini kama viongozi wa vyama vya upinzani nchini wanatumika na mataifa ya nje kuikwamisha serikali kufanya shughuli zake ninachokiamini ni ulimbukeni wa siasa ndio unaowasumbua na kuwashauri waachane na ujinga huo na kuungana na serikali katika kuijenga nchi yetu.
ReplyDeleteBIG UP..ninachokiamini ni ulimbukeni wa siasa ndio unaowasumbua na kuwashauri waachane na ujinga huo na kuungana na serikali katika kuijenga nchi yetu.
ReplyDelete