
Mamia ya wanawake wamemiminika leo katika ofisi hizo kufuatia wito wake kuwataka wanawake wote waliotelekezewa watoto na wazazi wenzao wa kiume wafike ofisini hapo na vielelezo halali ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria.
Wanawake hao ambao kwa sasa wanalea watoto wao peke yao baada ya kutelekezwa, wamejitokeza kuanzia majira ya asubuhi japo kuwa mvua kubwa zilikuwa zikinyesha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiria ameandika; Dar Es Salam Mpya! Wanawake tuliotelekezwa tunalea familia peke yetu!
Makonda ameanza rasmi kusikiliza shida za wanawake hao leo Aprili 9, 2018 ofisini kwake.