Mambo ni Hivi Joyce Kiria Naye Aenda Kumshitaki Mumewe kwa Kuwatelekeza Watoto

Mambo ni Hivi Joyce Kiria Naye Aenda Kumshitaki Mumewe kwa Kuwatelekeza WatotoMwanaharakati wa masuala ya usawa wa kijinsia na Mtangazaji wa kipindi cha ‘Wanawake Live’, Joyce Kiria ‘Super Woman’ (mwenye hereni pichani) amekuwa mmoja ya mamia ya wanawake waliojitokeza leo, Aprili 09, 2018 kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupatiwa msaada wa kisheria baada ya kutelekezewa watoto na wazazi wenzao.M


Mamia ya wanawake wamemiminika leo katika ofisi hizo kufuatia wito wake kuwataka wanawake wote waliotelekezewa watoto na wazazi wenzao wa kiume wafike ofisini hapo na vielelezo halali ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria.

Wanawake hao ambao kwa sasa wanalea watoto wao peke yao baada ya kutelekezwa, wamejitokeza kuanzia majira ya asubuhi japo kuwa mvua kubwa zilikuwa zikinyesha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiria ameandika; Dar Es Salam Mpya! Wanawake tuliotelekezwa tunalea familia peke yetu!

Makonda ameanza rasmi kusikiliza shida za wanawake hao leo Aprili 9, 2018 ofisini kwake.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad