Manesi Waliofukuzwa Kazi Watoa Huduma Bure Mbele ya Viwanja vya Bunge

Manesi Waliofukuzwa Kazi Watoa Huduma Bure Mbele ya Viwanja vya Bunge
Manesi takriban elfu 16 waliofukuzwa kazi kwa mgomo nchini Zimbabwe wametoa huduma bure kwa watu mbele ya viwanja vya bunge la nchi hiyo, kupinga kitendo chao cha kufukuzwa kazi.


Akizungumza na waandishi wa habari nchini humo mmoja wa manesi hao Pretty Mugudza, wamesema wameona ni vyema kufanya hivyo ili kuonyesha kuwa wanajali uhai na afya za watu, lakini kugoma kwao walichokuwa wakitaka ni kuboreshewa mazingira ya kazi, kwani wanashindwa kuvumilia kuona wagonjwa wakifa kwa kushindwa kuwapa huduma kutokana na kukosa nyenzo.

“Tunafanya hivi kuonyesha tupo kwa ajili ya watu, tunachoomba sisi ni mazingira mazuri ya kufanya kazi, hatuwezi kuangalia wagonjwa wakifa hospitali kwa sababu hatuna nyenzo, tunataka kufanya kazi lakini tumezuiwa kuingia kwenye vituo vyetu vya kazi”, amesikika nesi Pretty Mugudza,.

Waziri wa Afya wa Zimbabwe  David Parirenyatwa amesema kwamba hawawzi kuwarudisha manesi hao, lakini kama wanataka kufanya kazi watume tena maombi ya kazi.

Shirikisho la Manesi nchini humo limesema mpaka sasa manesi hao hawajapokea barua yoyote kuonyesha kuwa wamefukuzwa rasmi kazi.

Menesi hao walianza mgomo Jumatatu ya April  16, 2018 wakitaka serikali kuwaboreshea mazingira ya kazi, lakini serikali iliwafukuza kazi baada ya kugoma kurejea kazini licha ya kukubali kutatua changanoto zao na kuongeza kiasi cha pesa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad