Masiki Mama Kanumba Maisha Yazidi Kumchachia Aomba Msaada kwa Mzungu

Masiki Mama Kanumba Maisha Yazidi Kumchachia  Aomba Msaada kwa Mzungu
KUTOKANA na hali ngumu ya maisha hivi sasa, mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mahiri wa Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amemwangukia mwanadada mwenye asili ya kizungu aitwaye Mouna ili amsaidia kwenye shughuli ya kumbukumbu ya mwanaye inayofanyika kila Aprili 7.

Akizungumza na Over Ze Weekend, mama Kanumba aliweka wazi kuwa, amezunguka huku na kule, lakini hajapata msaada wowote hivyo anamuomba Mouna asimtupe kwenye hilo.

“Nimeona nimuombe tena Mouna kwa sababu alikuja Tanzania kuniona na kufika kaburini kwa Kanumba hivyo anaonekana wazi ana mapenzi kiasi gani na mimi na sasa ninamuona kama mwanangu,” alisema mama Kanumba.

Hivi karibuni, Mouna alitinga Bongo akitokea nchini Ujerumani na kufika kaburini kwa Kanumba kisha kwenda nyumbani kwa mama wa jamaa huyo, Kimara- Temboni jijini Dar na kuahidi kumchukua akapumzike kidogo kwenye nchi hiyo iliyo barani Ulaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad