Masogange Azidi Kumtesa Rammy Galis Pale Anapoona Jeneza Lake

Masogange Azidi Kumtesa Rammy Galis Pale Anapoona Jeneza Lake
KUFUATIA msiba wa msanii Agnes Gerald ‘Masogange’, msanii mwenzake Rammy Galis amekuwa mtu wa huzini, kulia na majonzi mazito hasa wakati anapoona jeneza lenye mwili wa marehemu.



Baada ya mwili wa marehemu kufika nyumbani kwao maeneo ya Utengule, Mbalizi mkoani Mbeya, msanii huyo alionekana kukosa raha na huku wasanii wenzake wakimsihi apunguze mawazo na ajipe moyo hasa katika kipindi hiki cha majonzni.



Rammy ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Masogange, jana alianguka na kuishiwa nguvu wakati akiaga mwili wa marehemu katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.



Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngomakilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao ambako amezikwa leo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad