“Zoezi linaloendelea hivi sasa kwa baadhi ya Mawaziri kutoa majibu ya hoja za CAG ni kinyume cha sheria , Sheria ya ukaguzi wa umma kifungu cha 38 (1), (2) kinaeleza utaratibu wa namna ambavyo hoja za ukaguzi zinapaswa kujibiwa na Mawaziri hawatajwi kabisa katika kifungu hicho” –Zitto Kabwe
“Wanaopaswa kujibu ni Makatibu wakuu wa Wizara na sio kujibu kwa kuita mikutano na Waandishi wa habari, hiki kinachofanyika na Mawaziri ni kinyume cha sheria na sheria imeweka adhabu kwa makosa hayo ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili jela au faini ya Shilingi Milioni tano” –Zitto Kabwe VIDEO: