Mchezo
huo ambao uligubikwa na vurugu za hapa na pale ulishuhudia wageni
Yanga, wakifunga bao la kuongoza dakika ya 57 kupitia kwa kiungo Raphael
Daud ambaye amesajiliwa msimu huu kutoka Mbeya City.
Bao hilo lilisababisha vurugu za mashabiki lakini baadae walitulia na mchezo ukaendelea hadi dakika ya 67 ambapo mlinzi wa kati wa Mbeya City Ramadhan Malima kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Juma Abdul.
Mashabiki walianza kurusha mawe uwanjani na kupelekea Jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi kuweza kutuliza vurugu hizo na mchezo kuendelea. Mbeya City waliendelea kucheza pungufu.
Tukio la mvuto zaidi katika mchezo wa leo ni bao la kusawazisha la Mbeya City ambalo limefungwa dakika ya 90 na mshambuliaji ambaye aliingia akitokea benchi na kufunga bao hilo ambalo limeamua mchezo umalizike kwa sare.