Mbeya Yasimama Mamia Wajitokeza Kuupokea Mwili wa Masogange

MAMIA ya wananchi wakazi wa Utengule, Mbalizi na maeneo ya karibu wamejitokeza kuungana na familia, ndugu, jamaa, marafiki na wasanii kuupokea mwili wa msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ ambao umewasili kijijini kwao kwa ajili ya mazishi.

Mwili wa marehemu umewasili kijijini hapo mapema leo baada ya jana kuagwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngomakilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao kuzikwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad